Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipanda ngazi katika
Kivuko cha Msanga Mkuu MV Mtwara kwa ajili ya kufanya ukaguzi wake leo
mjini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wa kwanza kulia akipewa
maelezo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kuhusu
ujenzi wa kivuko cha Msanga Mkuu(MV Mtwara) kilicho katika hatua za
mwisho za matengenezo chini ya Kampuni ya Sangoro Marine Transpot
Limited.
Mratibu
wa Mradi wa Daraja la Kigamboni kutoka NSSF Mhandisi Karim Mataka wa
kwanza kutoka kulia akitoa Maelezo ya maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa
Daraja la Kigamboni kwa Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt.John Pombe
Magufuli wakati wa ukaguzi wa Daraja hilo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mratibu wa Mradi
wa Daraja la Kigamboni kutoka NSSF Mhandisi Karim Mataka pamoja na
viongozi wengine kutoka Wizara ya Ujenzi wakiendelea na ukaguzi wa
daraja la Kigamboni kama inavyoonekana.
Luteni
Kanali Abel Gwanafyo akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ukarabati wa Kivuko cha MV. Kigamboni
kinachofanyiwa ukarabati na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kupitia kikosi
cha Wanamaji (Nav) Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka katika kivuko cha MV. Kigamboni mara baada ya Ukaguzi.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia akizungumza na
wakazi wa Kigamboni kuhusu ukarabati wa Kivuko cha MV Kigamboni. Dkt.
Magufuli aliwasihi wananchi hao kuwa wavumilivu kwani baada ya wiki
mbili Kivuko hicho kitakuwa tayari kwa kazi ya kuwavusha watu kama
kawaida.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisubiri Kivuko cha MV
Magogoni kwa ajili ya kuvuka mara baada ya kuzungumza na wakazi wa
Kigamboni kuhusu ukarabati wa Kivuko cha MV Kigamboni.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipanda kwenye kivuko
cha MV Magogoni mara baada ya kuzungumza na wakazi wa Kigamboni kuhusu
ukarabati wa Kivuko cha MV Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akitoka kwenye
kivuko cha MV Magogoni mara baada ya kuvuka kutoka Kigamboni
alipowahutubia wakazi wa Kigamboni kuhusu ukarabati wa Kivuko cha MV
Kigamboni jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment