Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Tuesday, September 9, 2014

WATU WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI LA MTU MMOJA KATI YA WATU WALIO POTEZA MAISHA KATIKA AJALI ILIYO TOKEA MUSOMA

Kaburi la mmoja kati ya watu waliopoteza maisha katika ajali mbaya iliyohusisha mabasi ya Mwanza Coach na J4 katika eneo la Sabasaba, Musoma, Mara limekutwa likiwa limefukuliwa na watu wasiojulikana leo asubuhi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichofika katika eneo la makaburi ya Musoma Basi, ndugu wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Juma Sai walienda asubuhi kuangalia kaburi ikiwa ni siku ya tatu tangu wafanye mazishi, ndipo walipokuta kaburi limefukuliwa na mbao zilizotumika kuhifadhi mwili kwa imani ya dini ya kiislamu zikiwa zimewekwa pembeni.
“Mwili wa marehemu bado uko ndani, watu wengi wako hapa na polisi wameimarisha hali ya usalama. Madaktari wameshafika hapa na wanafanya uchunguzi kuona kama kuna kiungo chochote kilichotolewa kwenye mwili wa marehemu. Inasikitisha sana.” Kimeeleza chanzo chetu cha kuaminika.
Ijumaa iliyopita, kulitokea ajali mbaya iliyohusisha magari matatu, mabasi ya kampuni ya Mwanza Coasch na J4 pamoja na gari dogo aina ya Landcruiser. Watu zaidi ya 40 walifariki na wengine 79 kujeruhiwa.
CHANZO: TIMES FM

No comments:

Post a Comment