Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Tuesday, September 9, 2014

KABURI LA MUME LAFUKULIWA BAADA YA MAHAKAMA KUAMURU HUKO MOSHI

Wachimabji wa Kijiji cha Mandaka wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro wakifukua Kaburi la Marehemu Stephen Assey  jioni hii kwa amri ya mahakama.
Askari Polisi wakisimamia zoezi la ufukuaji wa Kaburi hilo.
Msalaba uliokuwepo kwenye Kaburi hilo ukiwa pembeni.

Na Dixon Busagaga

Uamuzi wa kufukuliwa kwa kaburi hilo umefikiwa baada ya mke anayedaiwa kuwa ni wa ndoa wa marehemu Stephen Assey, Bi. Lucy Laurant kwenda mahakamani kuweka zuio la kuzikwa kwa marehemu katika eneo ilipo nyumba aliyokuwa akiishi na mke mdogo aliyefahamika kwa jina la Fortinata Lyimo.

 Kutokana na hali hiyo mahakama ya Hakimu mkazi Moshi iliamuru kufukuliwa kwa kaburi na mwili kuhifadhiwa hosptali hadi pale uamuzi wa mwisho utakapofanywa na mahakama hiyo. 

Globu ya Jamii kama kawaida yake itaendelea kuwapasha kila kitachojiri baada ya hatua hii ya kisheria.

No comments:

Post a Comment