Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Friday, December 5, 2014

WAZIRI WA UCHUKUZI DK .HARRISON MWAKYEMBE AZINDUA JENGO LA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (wa tatu kutoka kulia) Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kudumu ya Miundombinu, Peter Serukamba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar,  Dk. Juma Akir (kushoto) Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafii wa Anga Tanzania(TCCA) Dk. Nyamajeje Weggoro, wakishirikiana kukata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la TCAA. Uzinduzi huo ulikua sehemu ya maadhimisho ya Siku yaKimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Charles Chacha (Kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani(ICAD) yaliyofanyika kwenye viwanja vya TCAA.  Katiti ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Peter Serukamba.
Waziri wa uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe (Katikati)  Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar,  Dk. Juma Akir,( kushoto) Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu Peter Serukamba ,Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafii wa Anga Tanzania(TCCA),  Dk. Nyamajeje Weggoro (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Charles Chacha, wakishangilia baada ya kuzindua jengo la TCCA wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani(ICAD) yaliyofanyika kwenye viwanja vya TCCA jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe, akizindua jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA). Uzinduzi huo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani(ICAD). Anayeshuhudia kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu TCAA, Bw. Charles Chacha.

No comments:

Post a Comment