Madawa ya hospitali yakishushwa kwenye gari ili kuteketezwa.
Tukio
hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni mjini hapa ambapo paparazi
wetu alitonywa kuhusiana na kuwepo kwa ishu hiyo ambapo alikwenda na
kushuhudia lori lenye uzito wa tani 7 likisomba dawa hizo zilizoharibika
kwa awamu nne mfululizo na kwenda kutupa katika dampo lililopo maeneo
ya Kihonda-Viwandani.
Madawa yakitolewa kwenye viroba kuteketezwa.
Kwenye
uteketezaji huo, mwanahabari wetu aliwashuhudia baadhi ya maafisa wa
hospitali hiyo waliokuwepo kwenye dampo hilo wakitaka tukio hilo
lirushwe katika vyombo vya habari lakini wengine wakakataa na kudai
libaki kuwa siri.
Ilidaiwa
kuwa baadhi ya maofisa waliokuwa wanataka jambo hilo liwe siri,
walikuwa wakihofia kunyimwa dawa mpya na Bohari Kuu ya Taifa (MSD).
Maaskari wakisimamia zoezi hilo.
Mwanahabari
wetu alipohoji sababu za baadhi ya maofisa hao kutaka kulificha tukio
hilo, walimjia juu na kumtaka afute picha za tukio hilo lakini jitihada
zao zikagonga mwamba kwani paparazi wetu alifanikiwa kuwatoka.
WAKATI
wagonjwa wakifa kwa kukosa dawa hata kidonge kimoja kwenye hospitali
mbalimbali nchini, katika hali ya kushangaza, shehena kubwa ya madawa
katika Hospitali Rufaa ya Morogoro imeteketezwa kwa moto baada ya
kuharibika kwa kupita muda wake wa matumizi, Ijumaa Wikienda linakuwa la
kwanza kukujuza.
Baadhi ya dawa zilizowekwa tayari kuteketezwa.
Baadhi
ya mashuhuda wa tukio hilo walihoji kulikoni kuwe na shehena kubwa ya
madawa yaliyoharibika wakati wamekuwa wakitaabika wakiambiwa dawa hakuna
mara kwa mara wanapokwenda hospitalini hapo?
Katapila
likiandaa shimo kwa ajili ya kufukia madawa hayo.Alipotafutwa Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Godfrey Mtei na kuhojiwa
kuhusiana na tukio hilo, alikiri kutokea na kudai dawa hizo zilikuwa
zimeisha muda wake wa matumizi na hakukuwa na namna yoyote zaidi ya
kuziteketeza kwa moto.
“Ni utaratibu wetu, dawa zikiharibika huwa tunaziteketeza kwa moto,” alisema Mtei
No comments:
Post a Comment