Mgeni rasmi Hamad Rashid ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF akizunguza na wanafunzi
walioudhuria kwenye siku ya Career Day iliyofanyika kwenye viwanja vya chuo cha
Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam
Rais
wa Serikali ya Wanafunzi Katika Chuo cha Biashara,(CBE),Ramadhani S
Kirungi akiwakaribisha wageni mbalimbali katika siku ya "CAREER DAY"
iliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Jijini Dar es salaam
Afisa
wa PSPF Hadji Jamadary akiwa anafafanua na kuelezea kuhusu na
uchangiaji wa hiari wa PSS kwa wanafunzi wa Chuo Cha Biashara (CBE)
jijini Dar es salaam
Maseko
Kodalo Afisa wa Mfuko wa pensheni Wa PSPF akiwa anatoa maelekezo ya
kujiunga na mfuko huo kwa mpango wa lazima, Mikopo ya Elimu na mikopo ya
kuanzia maisha.
Mgeni rasmi Mh. Hamad Rashid ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF akitolewa ufafanuzi kufusu kazi za mfuko wa PSPF na Afisa wa PSPF Hadji Jamadary (wa pili kutoka Kushoto)
Mgeni rasmi Mh. Hamad Rashid ambaye ni Mbunge wa Jimbo la
Wawi kupitia CUF akipata ufafanuzi kutoka kwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha
biashara (CBE) wa kozi mbalimbali kuhusu kazi zao na maendeleo ya masomo yao.
Afisa wa PSPF Hadji Jamadary akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wanafunzi waliotembelea banda la mfuko wa PSPF.
Wanafunzi wakiwa kwenye banda la Mfuko wa PSPF wakipatiwa elemu kuhusu mikopo ya kuanzia maisha na fao la elimu.
Afisa wa mfuko wa Pesheni (PSPF) Abdalah Ahamed akitoa maelekezo kwa mmoja wa wateja
Wanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE) jijini dar es Salaam wakijaza fomu za kujiunga na mfuko wa PSPF
Baadhi ya washiriki ya washiriki wa Cereer Day
Baadhi
ya wanafunzi walioweza kutembelea banda la PSPF na kuweza kulimishwa
juu ya fao la elimuna mikopo ya kuanzia maisha wakitizama mtandao wa
Mfuko huo kwa njia ya simu
Mgeni Rasmi na PSPF wakiwa kwenye picha ya pamoja
na Baadhi ya viongozi wa Chuo cha Biashara (CBE) jijini Dar
Mbunge wa Jimbo la Wawi
kupitia CUF Mh.Hamad Rashid ameupongeza mfuko wa pensheni wa PSPF
kwa kuwa wadhamini katika Career Day ya Chuo cha biashara (CBE) iliyofanyika
katika viwanja vya chuo hicho siku ya ijumaa ambapo mbunge huyo aliweza kuwa
mgeni rasmi wa tukio hilo na kuwapa hongera PSPF kwa kitendo cha kuweza kuwa
pamoja na wanafunzi kwa ajiri ya kuwaandaa kuwa washiriki wazuri katika
uchangiaji wa mafao mbalimbali na kuweza kupata mikopo ya elimu na ile ya kuanzia maishi
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Katika Chuo cha Biashara,(CBE) Bw.Ramadhani
S Kirungi amewashukuru wanafunzi wote walio weza kushiriki katika
sherehe hizo kwani ni za kwanza toka chuo hicho kianze yapata miaka
hamsini (50) hazijawahi fanyika lakini katika uongozi wake amepata
bahati ya kuweza kuifanya siku hiyo, pia amewapongeza wanafunzi wa kozi
mbalimbali walio weza kufanya maonesho katika viwanja vya chuo hicho
kwaajiri ya kuwaonesha wahudhuriaji ufasaha wa masomo yao.
Pia
Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Maafisa wao walio weza kujitoa kwa
ajiri ya kuwapa elimu ya jinsi na namna ya kujiunga na mfuko huo
hususani katika fao la elimu na fao la kuanzia maisha ambapo ni mfuko
mojawapo wenye manufaa makubwa kuliko mifuko mingine unaoweza kutoa
huduma kulingana na mahitaji wa watanzania pasipo na ubaguzi wala
upendeleo
Maseko
Kodalo Ambaye ni Afisa wa Mfuko wa pensheni Wa PSPF yeye aliweza kutoa
rai kwa wanafunzi wote na wananchi wote waweze kujiunga na mfuko huo ili
kuweza kupata mafanikio, alitoa mifano michache ambayo inawezekana
ukaimudu pindi unapo jiunga na mfuko huo ambapo kwa mwanafunzi alitaja
kuwa unaweza kupata mikopo na kujiwekea akiba ili kuweza kukusaidia
katika masomo, vilevile kuna mikopo ya kuanzia maisha ambayo
itakuwezesha kupata nyumba ambazo wamezijenga kwa ajiri ya mtanzania
aweze kununua au kukopeshwa na baadae kuweza kurejesha mkopo huo
wanyumba, pia aliongeza kwa kusema nyumba zote zimewekewa bima endapo
tatizo lolote likitokea basi nyumba hizo zitakuwa salama .
No comments:
Post a Comment