
Mwenyekiti
wa Kamati ya Shule
ya Msingi Udasi mwambao mwa Ziwa Tanganyika, kata ya Kabwe wilayani Nkasi mkoani Rukwa,
Ismail Ndomboya (42) amenusurika kuuawa na mamba kwa kupambana kijasiri na
mnyama huyo kwa zaidi ya nusu saa.
Hata hivyo,
licha ya kuokoa maisha yake mnyama huyo katika mapambano
hayo alimng’ata na kumnyofoa mkono wake wa
kushoto na kutokomea nao ziwani.
Diwani
wa Kata ya Kabwe, Asante Lugwisha
akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu
alithibitisha kutokea kwa mkasa huo uliotokea juzi saa moja
na nusu jioni wakati Ismail alipokuwa akioga
katika Ziwa Tanganyika kijijini Kabwe .
Akisimulia
mkasa huo, Diwani Lugwisha alibainisha kuwa jioni
hiyo ya tukio Ismail aliamua kwenda kuoga
ziwani wakati huo akiwa pekee ndipo
ghafla mamba alimvamia ghfla na kumuuma mkono wake wa
kulia.
“Kwa ujasiri mkubwa Ismail alipambana
kufa au kupona na mnyama huyo kwa nusu saa huku akipiga
yowe akiomba msaada lakini hakuna aliyejitokeza
kumsaidia kwa sababu sehemu aliyokuwa akioga ilikuwa mbali na
makazi ya watu,“ alieleza.
Aliendelea
kueleza kuwa hatimaye mamba aliunyofoa mkono wa kushoto
wa Ismail na kutokomea nao ziwani ndipo Ismail
alipokimbia kuelekea nyumbani kwake akiwa uchi.
“Baadaye nilitaarifiwa
kuwa Ismail ameshambuliwa na mamba wakati akioga ndipo
nilipofika nyumbani kwake, na tulijipanga tukamkimbiza katika Hospitali
Teule ya Wilaya (DDH) mjini Namanyere ambao tulifika saa nne
na nusu usiku ambako amelazwa kwa matibabu “ alieleza.
Mtaalamu
wa afya wa Hospitali ya Wilaya, ambaye alikiri kuwa si
msemaji, alikiri kupokelewa kwa mgonjwa huyo
aliyejeruhiwa na mamba ambapo aliielezea hali yake kuwa
inaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment