Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Tuesday, March 17, 2015

MTOTO AUNGUZWA VIBAYA KWA KISU CHA MOTO

Tukio lililosikika  kwenye Hekaheka ni ishu ya mtoto wa mpangaji aliyemuunguza mjukuu wa mwenye nyumba kwa bahati mbaya wakati akicheza na wenzake, baadae mzazi wa mtoto huyo alikuja na kupewa taarifa za tukio hilo na kisha kumfanyia ukatili mtoto huyo.
Akisimulia tukio hilo mtoto huyo amesema alikuwa akitoka nje akiwa amebeba sufuria ndipo mtoto huyo akatokea akiwa anakimbia na kugongana nae na kukuunguza kwa bahati mbaya kichwani, baadae akiwa uwanjani baba wa mtoto huyo alimuita na kwenda nae nyumbani na kuweka kisu jikoni na kumchoma nacho sehemu mbalimbali za mwili wake kama kulipiza kisasi.
Majirani baada ya kugundua tukio hilo waliamua kwenda kushtaki Serikali za mitaa kutokana na mama huyo kuogopa kutoa taarifa akihofia kufukuzwa kwenye nyumba hiyo, Polisi walifika eneo hilo watu wao wakaanza kuwarushia maneno, kutokana na wingi wao wakaamua kuondoka na kwenda kuchukua gari ya Polisi kwa ajili ya kumkamata mtuhumiwa.

No comments:

Post a Comment