Moto ukiendelea kuteketeza Bweni la Wavulana
(Mkwawa ) katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambapo chanzo chake
kimetajwa kuwa ni hitilafu ya umeme ambapo moto huo ulizuka majira ya saa 3
asubuhi february 29 mwaka huu wakati wanafunzi wakiwa madarasani.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa mwenye
suti akisaidiana na kikosi cha Zima moto kuuzima moto ulioteketeza
Bweni la wavulana katika shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya linalolaza
wanafunzi 95 February 29 mwaka huu ambapo hakuna
Muonekano wa bweni la Wavulana katika shule ya
sekondari Iyunga jijini Mbeya mara baada ya kuteketea kwa moto uliosababishwa
na hitilafu ya umeme majira saa3 asubuhi ambapo hakuna mwanafunzi yeyote
aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo ya moto. .
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Munasa
akizungumza na Walimu pamoja na wanafunzi (hawapo pichani )katika shule ya
sekondari Iyunga jijini Mbeya mara ya baada ya kukumbwa na tukio la kuungua kwa
moto kwa mabweni ya wavulana ya (Mkwawa) February 29 mwaka huu
Kamati ya ulinzi na Usalama wilaya ya
Mbeya na baadhi ya viongozi wakitizama athari zilizotokea mara baada ya
mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari Iyunga jijini Mbeya kuungua moto
uliosababishwa na hitilafu ya umeme February 29 mwaka huu .
Afisa elimu Mkoa wa Mbeya Charles Mwakalila
akizungumzia athari zilizojitokeza mara baada ya mabweni ya wavulana katika
shule ya sekondari ya Iyunga jijini Mbeya ambayo yaliteketea kutokana na
hitilafu ya umeme majira ya saa3 asubuhi wakati wanafunzi wakiwa madarasani .
Baadhi ya wanafunzi waliofanikiwa kuokoa vifaa
vyao kwa masaada wa watu wa zima moto wakiwa nje wakisubiri utaratibu mara
baada ya bweni lao kuteketea kwa moto.
No comments:
Post a Comment