Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiwasili
katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano
kuhusiana na tuhuma za shambulio la mwili kwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es
Salaam, Theresia Mbando. Mbunge huyo alinyimwa dhamana na kutupwa rumande.
(Picha na Francis Dande)
Halima Mdee (katikati) akiwa na
mbunge wa Bunda, Ester Bulaya (wa pili kushoto) pamoja na wafuasi wa Chadema
wakati akielekea mahabusu.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akisindikizwa na Ofisa wa Polisi,
nyumba yake aliyeshika faili kuelekea mahabusu baada ya kunyimwa dhamana katika
Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria wa Mbunge wa Kawe,
Halima Mdee, Prof. Abdallah Safari ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Bara akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, baada ya mbunge
huyo kunyimwa dhamana.
No comments:
Post a Comment