Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Wednesday, March 9, 2016

WATU WATATU WAFARIKI NA ZAIDI YA 16 WAJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MATATU BARABARA YA MANDELA JIJINI DAR LEO ASUBUHI



Muonekano wa Daladala hilo baada ya kugongana uso kwa uso la Lori lililokuwa limepakia Ng'ombe, eneo la Tabata Matumbi, Jijini Dar es salaam leo.
Askari wa Usalama Barabarani na baadhi ya mashuhuda wakiwa eneo la tukio.
Ajali iliyohusisha Magari matatu likiwemo Daladala ya abiria linalofanya safari zake kati ya Gongo la Mboto kwenda Ubungo, imetokea mapema leo asubuhi katika barabara ya Mandela eneo la Tabara Matumbi, Jijini Dar es salaam na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 16 kujeruhuwa vibaya sana na kukimbizwa hospitali ya Amana, Ilala kwa Matibabu.

Inaelezwa kuwa, Chanzo cha ajali hiyo, ni Lori lililobeba Mchanga ambalo liliikuwa kwenye mwendo kasi, kwenda kuligonga Daladala hilo kwa nyuma, hali iliyopelekea Daladala hilo kukosa mwelekeo na kwenda kugonga na Lori lingine lililokuwa limepakia Ng'ombe waliokuwa wakipelekwa Pugu Mnadani.

Jitihada za kuyatoa magari hayo zinafanyika sasa. Kama unaweza kutoitumia barabara hiyo asubuhi hii ni vema kuepuka msongamano
Baadhi ya Ng'ombe walikuwemo kwenye Lori hilo, wakiwa wamewekwa kando baada ya kuokolewa.
Kichwa cha Lori hilo, kikiwa Chini baada ya Ajali.

No comments:

Post a Comment