
Mwenyekiti
wa TLP taifa Dkt. Augustino Lyatonga Mrema amesisistiza ombi lake la kazi kwa
kumkumbusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
kwamba ampe kazi yoyote amsaidie kibarua kigumu alichonacho cha kuwahudumia
wananchi
Dkt.
Mrema ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na EATV kuhusu miaka 32 ya kifo
cha aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Edward Moringe Sokoine ambaye alihudumu
kwenye awamu ya kwanza ya Mwl. Julius Nyerere ambapo alifariki akiwa na cheo
cha waziri mkuu tarehe 12.04.1984 kwa ajali ya gari.
''Namkumbuka
Sokoine kama mtu wa watu aliyehudumia watu, aliyepambana na ufisadi na magendo
.Alikuwa anatenda haki kwa wananchi wote .
"Hata
mimi nilipokuwa waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu nilijaribu
kufanya kama yeye bahati mbaya sikufanikiwa kama yeye kwa sababu sikuwa waziri
mkuu au Rais''- Alisisistiza Mrema.
Kuhusu
Mrema kuomba kazi kwa Dkt. Magufuli
Mrema
alisema kwa kutambua rekodi yake ya utendaji kazi wa Rais Dkt. Magufuli, aliwahimiza wananchi wa
Vunjo wamchague kipindi cha kampeni na yeye akampigia kampeni na Rais akawaambia
wananchi wa Vunjo kwamba Mrema akikosa ubunge atapangiwa kazi nyingine ndiyo
hiyo wananchi wanaulizia.
Aidha
Mrema alisema kuna maeneo ambayo yeye anafiti siyo lazima apewe madaraka
makubwa
"Mimi
sihitaji ukuu wa mkoa au uwaziri, anipe kazi yoyote na nikionana naye
nitamkonyeza maeneo ambayo ninafiti ili nimsaidie kutumbua majipu."
Alisema Mrema
Hata
hivyo Dkt. Mrema alimpongeza Dkt. Magufuli kwamba ni mtendaji ambaye ameamua
bila kusukumwa kupambana na mafisadi na kwamba yeye ni alfa na omega na kazi
hiyo ameonyesha kwamba atafanya vizuri kuliko Sokoine na Mrema.
No comments:
Post a Comment