Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Thursday, April 14, 2016

NAPE NNAUYE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KATIKA MAZISHI YA MWANAMUZIKI NGULI NDANDA KOSOVO

 Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo. Nape Nnauye akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa mwanamuzi nguli wa muziki wa dansi Ndanda Kosovo ‘Kichaa’ kabla ya mazishi yake yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa mwanamuzi nguli wa muziki wa dansi Ndanda Kosovo ‘Kichaa’ kabla ya mazishi yake yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kwa heri Ndanda.
 Nyoshi El Sadat akiwaongoza wanamuziki wa bendi ya FM Academia wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi marehemu Ngongo Onawembo "Ndanda Kosovo".
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika foleni ya kuaga mwili wa marehemu Ndanda Kosovo.
 Baadhi ya wanamuziki waliojitokeza katika mazishi ya Ndanda Kosovo.
(Picha na Francis Dande)

No comments:

Post a Comment