Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Friday, June 24, 2016

NACTE YATOA WITO KWA UMMA NA WADAU WA ELIMU KUTOA MAONI YA UTENDAJI WAKE

Kaimu Katibu Mkuu wa  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dk .Adolf Rutayuga, (Kulia) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa ikitoa kwa Umma na wadau wa elimu kutoa maoni ya utendaji wake.Katikati ni Mkurugenzi Udhibiti Ubora Rasmalimali watu , Edmund Kinwasi na Kaimu Mkurugenzi  Idara ya  Ufuatiliaji  Tathimini na Uthibiti wa baraza hilo , Christina Kumwenda.

Na Mwandishi Wetu

Ikiwa ni sehemu ya kuazimisha wiki ya utumishi wa umma nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limeutaka umma na wadau wa elimu kutoa mrejesho juu ya huduma zinazotolewa na Baraza hilo ili kuweza kuboresha huduma zake.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Baraza hilo na kusainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dk .Adolf Rutayuga ilisema Baraza linatoa fursa hiyo ya pekee kuanzia tarehe 23 mpaka tarehe 27 mwezi huu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Baraza katika kipindi hicho kitapokea mrejesho juu ya utendaji wake na changamoto mbali mbali ambazo wadau wa elimu wanakutana nazo wanapota kupata huduma kutoka NACTE.

Zoezi hili litafanyika kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa nane mchana katika jengo la udahili NACTE makao makuu lililopo eneom la viwanda vidogo Mikocheni jijini Dar es Salaam jirani na Chuo Cha Kodi jijini Dar es Salaam. Kwa wale waliopo mikoani huduma hiyo itatolewa katika ofisi zetu za kanda,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilitaja ofisi za kanda zitakazopokea mrejesho ni pamoja na zile zilizopo mikoa ya  Arusha, Dodoma, Mbeya, Mtwara, Tabora, Mwanza na Zanzibar.

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, kwa lengo la kusimamia na kuratibu taaluma zitolewazo na taasisi na vyuo vva elimu ya ufundi nchini, ambavyo siyo vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki.

Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za uendeshaji mafunzo ili tuzo zitolewazo na taasisi na vyuo ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.

No comments:

Post a Comment