Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Friday, June 24, 2016

ZANA HARAMU ZA WAVUVI BWAWA LA ZIWA LA MUNGU ZACHOMWA MOTO

ZANA haramu za uvuvi zilizokuwa zikitumika kuvuma samaki Bwawa la Nyumba ya Mungu, lililopo wilayani Simanjiro, zikichomwa moto.

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mahmoud Kambona, alichoma zana hizo zinazodaiwa kuwa na thamani ya Sh. milioni 160.

Akizungumza na wakazi wa vijiji vya Nyumba ya Mungu vilivyopo Kata ya Ngorika na Magadini iliyopo Kata ya Msitu wa Tembo, Kambona alisema uteketekezaji wa zana hiyo umechukuliwa kulinda samaki katika bwawa hilo.

“Sasa hivi tutakuwa wakali na kusimamia bwawa hilo baada ya shughuli za uvuvi kusitishwa Juni 19,” alisema na kuongeza, “tunafunga bwawa hili kwa muda wa mwaka mmoja na mtu kuvua samaki,” alisema.

Alisema viongozi wa mikoa ya Kilimanjaro na Manyara waliridhia kufungwa kwa bwawa hilo kwa muda wa mwaka mmoja ili samaki waongezeke.

Aliwataka wavuvi katika bwawa hilo kutafuta vyanzo vingine vya mapato.

“Sasa hivi tukimkamata mvuvi anavua kwenye bwawa hilo watachukulia hatua za kisheria,” alisema.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Jackson Sipitieck, aliwapongeza wavuvi waliosalimisha zana zao na kuagiza majina yao yaandikwe ili wasaidiwe kupitia mfuko wa vijana na wanawake.

No comments:

Post a Comment