Katibu  Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest
Rwegasira amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Frank
Charles Msaki kutokana na makosa ya kufanya malipo hewa yaani kulipa 
posho ya chakula kwa watu ambao si askari.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizarani hapo ambayo nakala
tumeipata, Mhasibu Mkuu huyo Bw. Frank Msaki  anasimamishwa kazi kwa
kufanya malipo ya kiasi cha sh. 305,820,000  kama posho ya chakula kwa
watu ambao sio askari kwa kipindi cha kuanzia mwaka  wa fedha 2013/2014
hadi 2015/2016.
Meja Jenerali Rwegasira amesema kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na
Taratibu za Kijeshi  anayetakiwa kulipwa posho ya chakula yaani ‘ration
allowance’ ni askari peke yake na si mtu mwingine yeyote yule.
Meja Jenerali Rwegasira amesema anamsimisha kazi Mhasibu Mkuu huyo
tangu leo tarehe 9 Julai, 2016 ili kupisha uchunguzi ufanyike juu ya tuhuma
zinazomkabili.
Katibu Mkuu huyo amesema baada ya jalada la uchunguzi kufunguliwa
na Ukaguzi Maalumu kufanywa na Mkaguzi wa Ndani wa Jeshi la Polisi imebainika
kuwa mbinu mbalimbali zimetumika ili kufanikisha  malipo hayo hewa. 
No comments:
Post a Comment