Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Jerry Sabi (katikati)
akiongea na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali na kutoa taarifa ya awali
ya zoezi la kuhakiki wanafunzi wanufaika wa mikopo ya wanafunzi lililoanza Mei
30, 2016 na linaloendelea katika vyuo vya elimu ya juu nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Jerry Sabi (kushoto) akiongea na waandishi kadhaa wa habari mara baada ya kumaliza Mkutano na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali na kutoa taarifa ya awali ya zoezi la kuhakiki wanafunzi wanufaika wa mikopo ya wanafunzi linaloendelea katika vyuo vya elimu ya juu nchini.
WANAFUNZI 2,739 hawakujitokeza kuhakikiwa katika zoezi
la uhakiki wa wanafunzi kwenye Taasisi za elimu ya juu nchini lilifanywa
na Timu maalum iliypoundwa na Bodi ya Mikopo kuanzia tarehe 30 Mei, 2016 ambapo
hadi sasa zoezi hilo linaendelea.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Jerry Sabi wakati akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Amesema kuwa Katika zoezi la
uhakiki wa wanafunzi jumla ya taasisi 26 zimehakikiwa, ambapo uchambuzi wa
taasisi 18 umekamilika.
Amesema zoezi la kuhakiki wanafunzi linaendelea katika
vyuo mbalimbali hapa nchini wataza na Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Chuo Kikuu
cha Kimataifa cha Kampala, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yosefu, Chuo cha Biashara –
Dar es salaam, Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Chuo Kikuu cha Mwenge, Chuo cha
Biashara - Dodoma na Chuo Kikuu cha Ushirika - Moshi.
Pia Bodi ya Mikopo imetoa wito kwa wanafunzi wote
ambao hawajahakikiwa kujitokeza haraka ili wahakikiwe kabla ya kuhitimisha
zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment