Chemba haribika ikiwa wazi maeneo ya Mwenge
Hapa ni chemba Hiyo ambayo ipo wazi na nipembeni ya barabara ya mwenge
Mawe yakiwa yamewekwa kuzuia magari yasipite hapo baada ya chemba hiyo kubomoka
Njia inayo leta mzozo kwa watumiaji wa magari wakati wa kukunja
Tatizo la chema za kupitisha maji taka likiwa lina sumbua jiji la dar es slaam leo katika pita pita tatizo hilo linezidi kuwakumba watu tofauti tofauti katika halmashauri ya kinondoni maeneo ya mwenge katika barabara ya lami eneo la pembezoni mwa kiwanja cha jeshi
hapo juu picha zinaonyesha Chemba iliyobomoka bila ya kufanywa marekebisho eneo hilo limekuwa kero na hatari kwa watumiaji wa barabara kwakuwa hiyo nisehemu ambayo magari huwa yana katisha kuelekea sehemu tofauti tofauti kupata huduma ikiwemo hospital
Barabara hiyo inayotumika kutoka mwenge kuelekea afrika sana.
Chemba hiyo ambayo ilibomoka baada ya gari la mizigo kutumbukia hapo na kusababisha kuharibika kwake.Mtandao wa Dj sek blog ulifanya mahojiano na waendesha bajaj na wafanyabiashara wa eneo hilo ambao walisema shimo hiilo limekuwa ni hatari kwa watumiaji wa barabara hiyo kwani kuna magari mengi yametumbukia hapo baada ya kupasuka kwa shimo hilo.
Waliongeza kuwa baada ya chemba hiyo kupasuka Dawasco walikuja wasafisha tu uchafu uliokuwemo humo na kuweka alama za tahadhari kisha wakaondoka.Sasa imepita takribani wiki moja sasa toka dawasco wameliona tatizo hilo lakini hakuna matengenezo yoyote ya chemba hiyo,pia wameongeza kwa kusema ifikapo jioni huwa shida sana kwa magari kupishana eneo hilo kwani magari yanayotoka afrika sana inabidi kukunja kwa kutumia upande wa magari yanayotoka barabara inayotoka kwa mama ngoma,hivyo kusababisha foleni kubwa na usumbufu.Watumiaji wa eneo hilo wameiomba manispaa ya Kinondoni kutatua tatizo hilo kwani mvua zinazoendelea kunyesha zitaleta madhara kwa kuwa chemba hiyo itakuwa inamwaga maji machafu nje ambayo itapelekea kuwapo kwa magonjwa ya mlipuko.
Chanzo;Dj sek blog
No comments:
Post a Comment