Social Icons

HII

WASILIANA NASI KUPITIA. E-mail: ngambabakari@gmail.com., Namba ya simu +255 657 185 504 Pia waweza kutujuza kwa lolote linalo endelea sehemu uliyopo

kachumbari

kachumbari

Thursday, April 9, 2015

WATU 10 WAMEFARIKI DUNIA KWA AJALI MKOANI TANGA ILIYOHUSISHA MAGARI MATATU KUGONGANA

 Basi la Ngorika likiwa halitamaniki baada ya kugongana uso kwa uso la basi lingine la Kampuni ya RATCO katika ajali iliyotokea mapema leo kwenye eneo la Kijiji cha Mbweni, Mkata mkoani Tanga.
 Hivi ndivyo lionekanavyo Basi la Ratco baada ya kupata ajali hiyo leo.
 Basi la Ngorika lionekanavyo baada ya ajali hiyo.
 Askari Polisi walifika eneo la tukio kwa Wakati ili kuhakikisha usalama unapatikana eneo hilo.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa, na inasikitisha sana.
 Kiukweli ajali hii ni yakusikitisha na kuhusunisha sana.
 Baada ya ajali ya Mabasi hayo, kulikuwa na gari hii iliyokuwa ikifuatana na moja mabasi hayo, na baada ya mabasi kugongana na gari hii ndogo ikaangukiwa na moja ya mabasi hayo.
Watu 10 wamefariki dunia kwa ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mkata kijiji cha Mbweni wilayani Handeni Mkoani Tanga majira ya saa 5 asubuhi ya leo. Wakati wa kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Tanga amesema kuwa “ajali hiyo imehusisha mabasi mawili ya abiria na gari dogo katika barabara ya Dar es salaa kwenda Tanga na Arusha”. Kwa mujibu wa Kamanda gari dogo ilikuwa likitaka kulipita lori lililokua mbele yake na ndipo ilipogongana uso kwa uso na basi la Ratco lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dar es salaam. Baada ya Basi la Ratco kugonganana na gari dogo, lilipoteza mwelekeo na kugongana tena uso kwa uso na basi la Ngolika lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Arusha. Aidha kamanda huyo amesema kuwa kati ya watu 10 waliofariki dunia wanaume watano akiwemo dereva wa gari dogo na dereva wa basi la Ngorika pamoja na wanawake watano wakiwemo watoto wawili.
picha na michuzi Media

No comments:

Post a Comment