Picha na Maktaba
Dereva mmoja mkoani Morogoro amefariki dunia wakati akijaribu kuvuka mto kwa gari wakati mvua kubwa ikinyesha.
Dereva huyo alikuwa akivuka mto huo ukiwa umefurika
maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali.
Kikosi cha jeshi la polisi linafanya uokozi wa kuopoa
mwili na gari lililozama katika mto ambapo mashuhuda wa tukio hilo wameiomba
serikali kuweka kingo za vyuma pembeni mwa daraja hilo ili kuzuia ajali za
kutumbukia magari.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba tukio hilo ni la kusikitisha
ambapo amewatahadharisha wananchi mkoani humo kuchukua tahadhari katika kipindi
hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini wakati
wanapovuka mito kutokana na mito mingi kujaa maji.
No comments:
Post a Comment