Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akizungumza na wanahabari kuhusu
kumvua madaraka Mhandisi wa Manispaa hiyo kwa kufanyakazi chini ya kiwango
pamoja na wasaidiziwake wawili.
 |
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akizungumza na wanahabari kuhusu
kumvua madaraka Mhandisi wa Manispaa hiyo, Japhery Bwigane na wasaidizi
wake wawili kwa tuhuma za kusimamia ujenzi wa barabara za manispaa hiyo kwa
kujengwa chini ya kiwango . Kulia ni Msaidizi wa Meya,
Semmy Mbegha.
|
Na Dotto
Mwaibale
MANISPAA
ya Ilala jijini Dar es Salaam imemvua madaraka Mkuu wa Idara ya ujenzi,
Mhandisi Japhery Bwigane na wasaidizi wake wawili kwa tuhuma za kusimamia
ujenzi wa barabara za manispaa hiyo kwa kujengwa chini ya kiwango.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam wakati akitoa taarifa hiyo, Mstahiki Meya
wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko aliwataja maofisa wengine wa idara hiyo
waliosimamishwa kuwa ni Siajari Mahili na Daniel Kirigiti ambao wamehamishwa
idara hiyo ili kupisha uchunguzi unaoendelea.
Kuyeko
alisema kikao cha Baraza la Madiwani kimefikia uamuzi huo baada ya
manispaa kujiridhisha kuwa maofisa hao wamechangia kwa kiasi kikubwa ujenzi wa
barabara mbovu ndani ya manispaa hiyo.
Alisema
baada ya kuingia madarakani kwa miezi mitatu walijaribu kutafuta kero ndani ya
manispaa ya Ilala ambapo walibaini idara ya ujenzi ina malalamiko mengi kutoka
kwa madiwani wa kata mbalimbali kwa sababu ya kusimamia ujenzi wa barabara
chini ya kiwango na hakuna hatua stahiki zilizochukuliwa na maofisa hao.
Alisema
madiwani hao walimlalamikia Mhandisi Bwigane kuwa amekuwa akikaidi wito wao wa
kujadili ujenzi wa barabara mbovu pindi zinapobainika jambo ambalo
limesababisha manispaa hiyo kuwa na barabara nyingi mbovu.
Jitihada
za gazeti hili za kumtafuta Mhandisi Bwigane ili kuzungumzia kusimamishwa kwake
kazi hazikuzaa matunda baada ya kupigiwa simu yake na wakati wote kuwa
imefungwa.
(Imeandaliwa
na mtandao wa www. habari za jamii.com)
|
No comments:
Post a Comment